<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><hymn_number>102</hymn_number>
<lyrics>[V1]
 Kazi yangu ikiisha, nami nikiokoka;
 Na kuvaa kutokuharibika,
 Nitamjua Mwokozi nifikapo ng'amboni;
 Atakuwa wa kwanza kunilaki.

[V2]
 Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
 Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.

[V3]
 Furaha nitapata nikiona makao
 Bwana aliyotuandalia;
 Nitamsifu mwokozi kwa rehema na pendo
 Vilivyonipa pahali Mbinguni.

[V4]
 Nao waliokufa katika Bwana Yesu,
 Nitawaona tena huko juu;
 Lakini nifikapo kwake huko Mbinguni,
 Nataka kumwona Mwokozi kwanza.

[V5]
 Milangoni mwa mji Bwana atanipitisha,
 Pasipo machozi wala huzuni.
 Nitauimba wimbo wa milele; lakini
 Nataka kumwona Mwokozi kwanza.</lyrics>
<title>Kazi Yangu Ikiisha TZR102</title>
</song>